Serikali yakiri kuona mchango wa Maendeleo ya Wanawake nchini
Na Mwandishi wetu
Serikali imesema kuwa maendeleo ya wanawake yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa Kati.
Kauli hiyo imetolewa katika viwanja vya mpira Ngarenaro na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh.Jerry Muro wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Idd Kimanta kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa Wanawake wa Jiji la Arusha
Mh.Muro alisema kuwa wanawake wanajituma katika nyanja mbali mbali na kwamba kwa sasa kwa kiwango kikubwa wanaongoza kiuchumi.
Pamoja na mambo mengine alipongeza wanawake Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa umoja wao nakuwataka kuendelea kufanya shughuli zao kwa bidii na kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono.
Alisema Serikali itaendelea kutoa mkopo wa asilimia 10 kupitia Halmashauri ambao Wanawake pia ni wanufaika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kehongosi akimkaribisha kaimu Mkuu wa Mkoa Mh. Jerry Muro katika sherehe hiyo alikiri kuwa Wanawake wanamchango mkubwa wa maendeleo na kwa Mh Rais Dk.John Pombe Magufuli anajali wanawake .
Mh.Kihongosi alisema kuwa anaunga jitihada za Mh. Rais Mkono na kwamba amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao bila bhuguza na kuwasaidia pindi wanapobainika wanaonewa.
Maadhimisho ya wanawake katika Jiji la Arusha yalipambwa na mada mbali mbali za kuwajenga na kuwajengea uwezo wa kujitambua.
PICHANI :MATUKIO YA SIKU YA WANAWAKE ILIVYOFANA KATIKA UWANJA WA MICHEZO WA NGARENARO JIJINI ARUSHA
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa