WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Arusha Girls katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wametakiwa kutumia vyema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili waweze kuendana na mabadiliko yanayotokana na kuendelea kukua kwa teknolojia hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Emanuel Mahundo wakati wa Makabidhiano ya msaada wa Kompyuta 25 zilizotolewa na Shirika la empower na KOICA.
Bw. Emmanuel Mahundo alisema kwamba elimu ya TEHAMA imekuwa chachu ya maendeleo kwani imekuwa ikirahisisha kazi ambapo aliwahimiza wanafunzi hao kutumia fursa hiyo ipasavyo iliwaletee manufaa katika maisha yao.
“Niwaombe mtumie elimu ya TEHAMA hasa Teknolojia ya mitandao kwa mambo yaliyo mema na sio mabaya kwa kuwa mkiitumia vibaya mtaua ndoto zenu zakufanya vizuri na kuishi maisha bora hapo baadaye” alisema Mahundo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Omary Kwesiga amewataka wanafunzi hao kutumia elimu ya TEHAMA kwa kuongeza maarifa zaidi ya kujifunza.
Kwesiga aliwataka kutunza vizuri vifaa hivyo ili vilete manufaa kwa wanafunzi waliopo na watakaokuja kujiunga katika shule hiyo ya wanafunzi wa sasa na watakaokuja kujiunga katika shule hiyo baadae.
Naye, Kaimu Afisa Elimu Jiji la Arusha, Ndg. Prosper Kessy amewashukuru wadau hao wa Kampuni ya empower na KOICA kwa msaada huo na kwamba kitendo hicho ni ishara kuwa wanajali na kutambua umuhimu wa elimu.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa