Karibuni katika Tovuti.
Tovuti ambayo itakupa mwanga wa kufahamu zaidi kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Jiji hili na kuleta maendeleo endelevu kwa Wananchi wake.
Kwa kifupi Jiji hili lilianzishwa miaka ya 1830 na kuendelea kukua kama Mji wa biashara hatimaye Mwaka 1948, Mji ulikuwa na wakazi 5320 na ukapandishwa hadhi kuwa Mamlaka ya Mji.
Watu waliendelea kuongezeka hivyo kuleta Mvuto wa Kijamii kutokana na ukarimu wa jadi na utamaduni imara wa wenyeji wa Arusha. Kasi ya kukua kwa Mji iliongezeka baada ya kupandishwa hadhi kuwa Manispaa Mnamo mwaka 1980 ukiwa na eneo la Kilometa za Mraba 93 na kuwa Jiji mwaka 2011.
Katika Kipindi hicho chote Jiji limeendelea kuhkikisha kwamba linatoa huduma bora kwa wananchi wake katika sekta ya Elimu, Afya, Miundombinu, uimarishaji wa biashara na Maendeleo ya Jamii.
Katibu kwenye Tovuti ya Jiji ili uweze kuifahamu zaidi Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa