Halmashauri ya Jiji la Arusha lina jumla ya ng’ombe 43,071 kati yao, ng’ombe 41,173 ni wa kisasa na ngo’mbe 1,898 ni wa kienyeji. Mifugo hii inahudumiwa na Majosho manne na kliniki nne za Mifugo. Pia kuna vituo vya uchunguzi wa maradhi yamifugo vinne(4).
Vilevile kuna viwanda vya kusindika nyama, maziwa na ngozi ambavyo vimekuwa na tija kubwa sana kwa wafugaji, kwani vimeongeza sana thamani ya mazao ya mifugo. Katika Jiji la Arusha kuna viwanda 2 vya kusindika maziwa na pia Halmashauri inamiliki Machinjio ya Kisasa ya ng’ombe (Arusha Meat Company) ambayo inaongeza ubora wa nyama Inayosambazwa katika masoko mbalimbali ndani na nje ya Jiji. Halmashauri ina kituo cha Rasilimali Mifugo(Live stock Resource Center) ambacho kinaendelea kuimarishwa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa