Jiji la Arusha limekuwa ni kitovu cha utalii ndani na nje ya Tanzania. Kuna jumla ya hoteli za kitalii zipatazo 20, kampuni za utalii 84 na pia ni kituo cha kuelekea kwenye maajabu matatu ya Dunia yanayopatikana katika Nchi yetu ambayo ni Mt. Klm, Ngorongoro na Serengeti.
Kituo cha mikutano cha Arusha International Conference Centre (AICC) kimechangia kwa kiasi kikubwa sana kukua na kuenea kwa shughuli za kitalii.
Sekta hii ya utalii ni muhimu sana kwa wakaazi wa Jiji, kwani imetoa nafasi nyingi za ajira kwa vijana na pia ni chanzo kikubwa cha mapato kwa Jiji na Wananchi kwa Ujumla.
BIASHARA
Jiji la Arusha limekuwa ni kitovu kikubwa cha biashara. Inakisiwa kuwa kuna jumla ya wafanyabiashara wapatao 7,500 wanaofanya shughuli mbalimbali za kibiashara.
Katika kuhakikisha kwamba, wafanyabiashara hawa wanakuwa na mazingira mazuri ya kufanyia biashara. Halmashauri imejenga masoko matano (5) ambayo ni soko la Kati, soko la Kilombero,soko la Kijenge, soko la Sanawari na soko Mjinga. Masoko mengine ya Shuma na Baraa yapo katika hatua mbalimbali za kukamilika.
Halmashauri imetekeleza haya yote ili kufanikisha adhma yake ya kusogeza huduma karibu na wananchi
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa