VIBALI VYA UJENZI
Imeandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi Jiji l Arusha Tarehe 20th August 2016
UTARATIBU WA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
Kibali cha Ujenzi ni kibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenzi mjini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wa jengo.Mwombaji wa Kibali cha ujenzi anapaswa ajaze fomu ya maombi ya kibali cha ujenzi B-PERMIT
Bofya hapa chini kupata fomu ya kibali cha Ujenzi.
Fomu ya Maombi ya Vibali vya Ujenzi.
UMUHIMU WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
•Kutimiza takwa la sheria ndogo za jiji
•Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yalivyoelekezwa katika mipango miji ya jiji
•Kudhibiti ujenzi holela
TARATIBU & KANUNI ZA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI
•Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na halmashauri ya jiji la Arusha yaabi “Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;
•Mkaguzi wa Majengo wa Jiji (Building Inspector)
•Afisa Ardhi wa Jiji (City land officer)
•Mpima wa Jiji (City Land surveyor)
•Afisa Mipango Miji wa Jiji (City Town Planning Officer)
•Afisa Afya wa Jiji (City Health and Sanitation Officer)
•Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na halmashauri Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “architectural & structural drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyoonyeshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki kama ifuatavyo;
Mkaguzi wa Majengo wa Jiji (Building inspector) - kuona kama michoro inakidhi haja ya kiufundi na specifications
Afisa Ardhi wa Jiji (City land officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.
Mpima wa Jiji (City Land Surveyor) – kutambua mipaka halali
iv.Afisa Mipango Miji wa Jiji (City Town Planning Officer) – Kuona kama ujenzi unaoombewa ni sahihi kwa mujibu wa michoro ya mipango miji, eneo la maegesho lipo, nk .
Afisa Afya wa Jiji (City Health and Sanitation Officer) – kuona kama usafi kwa ujumla na maji taka yatatunzwa vyema
Afisa Ardhi wa Jiji (City land officer) – kuona kama umiliki wa eneo linaloendeleza ni halali, kukagua hati miliki, nk.
•Kama michoro na nyaraka za umiliki zimekidhi vigezo zitawasilishwa kwenye kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali
•Baada ya michoro na nyaraka kupita katika kamati ndogo ya mipango miji na utoaji vibali itapigiwa makadirio na mwombaji atapaswa kulipia gharama husika kwenye akaunti ya benki 40801200336 - “council own source collection”
•Mwombaji kuandaliwa kibali cha ujenzi kinachosainiwa na mhandisi wa ujenzi na afisa mipango miji
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa