Halmashauri ya Jiji la Arusha imejipanga kuboresha vijiwe vya kunywea kahawa na wasafisha viatu (Shoe Shiner) kwa kuviongezea thamani.
Mpango huo umewekwa madhubuti kwa ajili yakuongeza vyanzo vya mapato vya halmashauri kwani kuboresha vijiwe hivyo kutasaidia kuongeza thamani na ubora wa biashara.
Akizungumza na wananchi wa kijiwe cha Kahawa maarufu kwa Issa katika Kata ya Sinoni Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe amesema lengo la halmashauri ni kuufanya mji huo wa Kitalii uendelee kuvutia wageni mbalimbali wanaofika katika shughuli za kitalii.
Amesema, pia mpango huo utasaidia kuongeza mnyororo wa thamani katika vijiwe vya Kahawa kwani huduma mbalimbali zitakuwepo kama vile; uuzaji wa Karanga na Kashata ambavyo vitaongeza pato la wajasiliamali hao.
Pia, amesema kuboresha vijiwe hivyo kutawafanya hata watalii waweze kupata huduma za Kahawa katika maeneo hayo na kusafisha viatu vyao kwa uhuru zaidi.
Vilevile, vijiwe hivyo vitaongeza mapato kwa halmashauri kutokana na huduma kuboreshwa na wataweza kupata wateja wengi.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Sinoni Mhe.Michael Kivuyo amesema maboresho ya vijiwe hivyo yataleta chachu kwa wananchi kwa kuona ni maeneo salama kwao na wataweza kukaaa kwa uhuru na kubadilishana mawazo.
Maboresho ya Vijiwe vya Kahawa na wasafisha viatu katika Jiji la Arusha kutosaidia kuufanya mji uwe msafi zaidi na kuwavutia watalii wengi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa