Timu ya netiboli ya Jiji la Arusha wameibuka mabingwa wa michuano ya mapinduzi Cup yaliyofanyikia katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar Tarehe 5-13 Januari 2020 ambayo yameratibiwa maalum kwaajili ya kuenzi miaka 56 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Afisa michezo Jiji Ndg. Benson ameeleza kuwa ni mara ya kwanza kwa Arusha kushiriki katika michuano hiyo kutokana na kufanya vyema katika ligi ya Tanzania bara mwezi agosti Jijini Dodoma kupelekea Arusha kuibuka mshindi wa tatu wakikomesha utawala wa takribani miaka 40 wa timu za majeshi.
Kocha wa timu hiyo Bi. Nauridine Hassan pia amesema Kwa sasa Arusha Jiji wanajiandaa na mashindano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi machi 2020 Jijini Kampala huko Uganda.
Katika mapokezi ya mabingwa hao kurejea nyumbani , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid S. Madeni amewapongeza wachezaji hao kwa kutwaa ubingwa na kuahidi kuwa Jiji litaendelea kutoa ushirikiano katika mashindano mbali mbali watakayo shiriki.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa