Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amefurahishwa na usimamizi wa ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashuri ya Jiji la Arusha.
Pongezi hizo alizitoa alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu, barabara na Maji.
Amesisitiza zaidi ukamilifu wa miradi hiyo kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika nayo kama Serikali ilivyopanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amesema miradi yote itakamilika kwa wakati kwani wakandarasi wote wanaenda kwa kasi inayotakiwa na ikibainika kuna Mkandarasi anazembea basi uongozi wa Halmashauri utamvuniia mkataba na kupatiwa mwingine.
Vilevile, amesema katika usimamizi wa matumizi ya fedha za miradi hiyo Halmashauri inaendelea kusimamia ili miradi iweze kukamilika kwa ubora unaotakiwa.
Nae, Diwani wa Kata ya Sekei Mhe. Gerald Sebastian amesema katika mradi wa ujenzi wa shule msingi Sekei majengo yanayojengwa ni Madarasa 8, Matundu ya Vyoo 8,Jengo la Utawala, Maabara 3,Darasa la TEHEMA na Maktaba moja.
Amesema kujengwa kwa shule hiyo ambayo inatarajiwa kukidhi mahitaji ya wakazi wa eneo la hilo na maeneo jirani kwa takribani miaka 100, hivyo itaweza kusaidia vizazi vingi.
Aidha, ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi huo na miradi mingine mingi katika kata hiyo na wanachi wameshaanza kuona matunda yake.
Diwani wa Kata ya Lemala Mhe. Nayosi Paulo ameishukuru Serikali kwa kuleta fedha takribani milioni 765 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Korongoni katika kata hiyo.
Amesema uwepo wa shule hiyo katika kata yake kutawarahisishia wanafunzi wengi kutotembea umbali mrefu kwenda kupata masomo yao.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa