Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha Dkt. Onesmo Mandike amesema kuna umuhimu wa elimu kutolewa zaidi kwa wazazi juu ya umuhimu wa utoaji wa chakula shuleni.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya lishe yaHalmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema wazazi wakielewa umuhimu wa lishe , itasaidia watoto wote kupata chakula cha mchana wakiwa shuleni.
Lengo la Serikali ni kuhakikisha watoto wanapatiwa chakula shuleni na kuwawezesha kusoma vizuri wakati wa mchana badala ya kutoroka na kurudi nyumbani kupata chakula na wengine kushindwa kurudi tena kuendelea na masomo yao.
Kwakufanya hivyo kutasaidia kuimarisha mifumo ya ufikiri kwa watoto hao na kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule zetu.
Sambamba na hilo ameshauri wananchi kulima mazao ya muda mfupi hasa kipindi hiki ambacho mvua hazijaanza kunyesha ili kuwawezesha kupata chakula cha kutosha.
Kwa upande wake afisa lishe Halmashauri ya Jiji la Arusha Namsifu Godson amesema katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 halmashauri imevuka lengo la utoaji fedha za lishe kwa watoto chini ya miaka 5 kutoka shilingi 2004 iliyopangwa kwa kila mtoto hadi kufikia shilingi 2159.
Amesema juhudi hizo zimepelekea kupata asilimia 107 ya afua za lishe katika kipimo cha kadi alama (score card) kwa robo ya kwanza kwa mwaka 2023/2024.
Vilevile,amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuisaidia Serikali katika utoaji wa elimu ya lishe katika nyumba zao za ibadi kwa kufanya kazi mbalimbali za kijamii na kuwaalika wataalamu wa lishe kutoa elimu hiyo.
Kamati ya lishe ya Halmashauri ya Jiji la Arusha imefanya tathimini yake ya maswala ya lishe kwa robo ya kwanza ya mwaka na kurithika na namna fedha za lishe zinavyotolewa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa