Takwimu hiyo imetolewa na Afisa Lishe Jiji la Arusha Bi. Rose Mauya alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya kitengo cha lishe wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 kilichojumuisha wajumbe wa kamati za lishe ngazi ya Wilaya .
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Arusha jana Tarehe 18, Otoba 2018, Bi. Rose ameyaelezea mafanikio ya shughuli za lishe kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuwa ni pamoja na wazazi na walezi 20, 543 wamenufaika na utolewaji wa elimu kuhusiana na mwezi wa lishe ya mtoto iliyotolewa katika vituo vyenye huduma ya mama na mtoto ambapo ilihusisha utoaji wa matone ya Vitamin A, utoaji wa vidonge vya kuondoa maambukizi ya minyoo na ufanyaji wa tathmini ya hali ya afya ya lishe.
Mafanikio mengine ni utolewaji wa elimu ya lishe kuhusiana na mlo kamili, mtindo bora wa maisha na magonjwa yasiyoambukiza kwa vikundi vya vijana na wanawake wakati wa mafunzo ya utolewaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali ambapo zaidi ya watu 156 walipatiwa elimu hiyo.
“Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 watoto waliokuwa na hali mbaya kilishe waliweza kubainika na kupatiwa huduma, sambamba na kuhakikisha wazalishaji wa bidhaa za vyakula wanazingatia umuhimu wa urutubishaji wa vyakula” aliongeza Bi. Rose
Naye mganga mkuu wa jiji la arusha ambaye ndiye katibu wa kamati ya lishe katika ngazi ya halmashauri Dr. Simon Chacha ameyaelezea maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji katika kipindi cha July – Septemba kwa mwaka huu wa fedha tulionao ambapo amesema kuwa maadhimisho hayo yalifanyika katika vituo vya kutolea huduma za afya na viwanja vya Nanenane ambapo ulifanyika upimaji wa hali ya afya kilishe na ufuatiliaji wa ukuaji wa watoto chini ya umri wa miaka mitano .
“Katika maadhimishi ya wiki ya unyonyeshaji tuliweza kutoa elimu ya unyonyeshaji kwa miezi 6 ya mwanzo kwa wazazi na walezi ambapo jumla ya wazazi na lezi wenye watoto wa umri wa miezi 0-6 waliopatiwa elimu hiyo ni 1,455, wazazi na walezi wenye watoto wa umri wa miezi 6-23 ni 2,235 na wazazi na walezi wenye watoto wa umri wa zaidi ya miezi 23 – 2,892” alisema Dr. Chacha.
Dr. Chacha aliongeza kwa kusema kuwa miongoni mwa jukumu kubwa la kamati ya lishe Jiji la Arusha ni kuendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe bora, kuelimisha wazalishaji waweze kujua madhara ya kutofanya urutubisaji wa vyakula na kufanya tathmini ya hali ya afya ya lishe pamoja na kuendelea kuwaelimisha wazazi na walezi juu ya umuhimu wa mwezi wa afya na lishe ya mtoto.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa