Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Gabriel Daqarro amemtaka Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Murriet, Bw. Mustafa Miraji Kuhakikisha huduma za wazee zinapewa kipaumbele ikiwemo kuwekewa dirisha lao maalum la dawa.
Dc Daqarro ametoa agizo hilo hapo jana wakati wa ziara yake katika kituo hicho kukagua maandalizi ya matumizi ya kituo hicho ambapo mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa jengo la wagonjwa wa nje na liko tayari kutumiwa na wananchi na huduma zimeanza kutolewa ikiwemo huduma ya mama na mtoto, huduma ya wagonjwa wa nje (opd), maabara, dawa na chanjo.
Wakati wa ziara yake katika kituo hicho dc daqarro aliwapongeza watumishi wa afya katika Jiji la Arusha, Mhandisi wa Jiji na kila mmoja kwa nafasi yake katika kufanikisha kukamilikwa kwa ujenzi wa kituo cha Afya Murriet na kuwataka watumishi katika kituo hicho kufanya kazi kwa weledi na kujitoa kwa ajili ya wananchi na kudhibiti matumizi ya dawa.
Pia amemwaagiza Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dkt. Simon Chacha kuhakikisha Mfumo wa malipo wa serikali unaanza kutumika mara moja ili kukwepa vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa Fedha za serikali.
“Makatibu wa afya fuatilieni madai na maslahi na madai ya watumishi na pia hakikisheni mnaendesha vikao vya mara kwa mara ili kubaini changamoto mbalimbali na kuongeza ufanisi wa kazi ” aliongeza Mkuu wa Wilaya huyo
Utolewaji wa huduma za afya katika kituo cha Murriet utasaidia kutatua changamoto za huduma za afya kwa wakazi wa kata ya Murriet na Jiji zima kwani utaimarisha hali ya utoaji wa huduma za afya na kupunguza msongamano katika hospitali na vituo vingine vya afya vilivyopo Jijini Arusha
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa