Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Sophia Mjema amesema hatawavumilia watumishi wazembe, wasiofuata haki na wasiojua wajibu wao na kwamba ataanza kufuatilia mtumishi mmoja mmoja ili kubaini utendaji wake.
Mkuu huyo ametoa kauli hiyo makao ya ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha wakati akizungumza na watumishi wa idara mbali mbali wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwa ni mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Alisema kuwa watumishi wa Serikali wanapaswa kuwa kioo cha Jamii kwa kufanya kazi yakutumikia wananchi kwa uadilifu na hatimaye kuwaletea maendeleo.
Dk.Mjema alisema kuwa atashirikiana na kila mtumishi kwamba ofisi yake iko wazi kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na watumishi wote wa Jiji la Arusha .
Alisema kuwa atamtea mtumishi mwadilifu ikiwa atabainika anaonewa na mtumishi mzembe atamchongea bila kumuonea haya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima alisema kuwa maagizo ya Mkuu wa Wilaya yatatekelezwa na kwamba watumishi wa Jiji la Arusha watampatia ushirikiano hatimaye kumuwezesha kutekeleza majukumu yake bila kikwazo.
Pamoja na mambo mengine alisema kuwa Jiji la Arusha linafanya vizuri katika Taaluma kwamba jitihada za kuboresha miundo mbinu ya elimu zinaendelea.
Awali Afisa Utumishi wa Jiji la Arusha Msena Bina alimwambia Mkuu huyo kuwa Watumishi wa Jiji la Arusha wanatekeleza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi katika idara zao na watumishi wazembe wanachukuliwa hatua za kinidhamu.
Bina anasema kuwa watampatia Mkuu wa Wilaya ushirikiano na kwamba nia ya Watumishi wa Jiji la Arusha ni kuhudumia kila Mwananchi bila ubaguzi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa