Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni amesema kuwa ifikapo kesho Tarehe 18 Januari, 2019 operesheni ya ukusanyaji wa mapato inatarajiwa kuanza upya baada ya kupumzika kwa muda mfupi kupisha msimu wa mapumziko na sikukuu.Ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake leo Taehe 17 Januari, 2019 ambapo ameitambulisha timu mpya katika awamu hii ambayo ni Wakuu wa Idara zote zilizoko Halamshauri ya Jiji la Arusha na kila mmoja ataambatana na watumishi walio chini yake na watapangiwa maeneo maalum ya usimamizi na ufatiliaji.“Lengo kubwa la kuendeleza operesheni hii ni kuongeza pato la Halmashauri yetu na malengo tuliyojiwekea ni kukusanya zaidi Bilioni 15.6 kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 badala ya Bilioni 13 tulizokusanya katika mwaka wa Fedha uliopita wa 2017/2018 hivyo operesheni hii itaendelea ili kutuwezesha kufikia malengo hayo”“Katika wiki za hivi karibuni mapato yamekuwa yakishuka siku hadi siku kufuatia watu kujijengea dhana mbaya juu ya vitambulisho vya machinga hivyo niwaombe walioko katika maeneo yao rasmi waendelee kufata sheria na taratibu za kawaida walizowekewa bila kuathiri mapatao ya Halmashauri na sisi tutaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili” alisema Dkt. Madeni.Aidha Dkt. Madeni aliwambia waandishi wa habari kuwa mpaka sasa wafanyabiashara wadogo 5770 wameshapatiwa vitambulisho na uhamasishaji unaendelea ili kufikia idadi ya wafanyabiashara 8000. Huu ni muendelezo wa operesheni yake ukusanyaji wa mapato aliyoianzisha Mwezi Octoba Mwaka2018 iliyolenga kuhakikisha wafanyabiashara wote na wamiliki wa vibanda wana leseni za muda husika, risiti halali za kodi na mikataba halali ya halmashauri sambamba na kufungia vibanda kwa wafanyabiashara wote ambao hawana vielelezo vya kutosha katika vyanzo vyote vya mapato ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha. MWISHO.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa