Chama cha Msalaba Mwekundu Nchini Tanzania (RED CROSS) Leo Tarehe 20/02/2019 Kimemkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni vifaa vya usafi, magodoro na mablanket kwa ajili ya kituo cha Afya Murriet kilichopo Jijini Arusha
Dkt. Madeni amekishukuru Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani Arusha kwa kujitolea vifaa hivyo kwakuwa vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha hali ya usafi katika kituo cha Afya Murriet sambamba na magodoro ya kulalia wagonjwa na mablanketi ya kujifunikia wagonjwa wawapo wodini.
“Nichukue fursa hii kuijulisha jamii kuwa Halmashauri yetu inatoa fursa ya kupokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali , sio tu katika sekta ya Afya bali katika sekta nyingine pia za maendeleo na kuboresha huduma za jamii kwa wakazi wa jiji la Arusha” Alisema Dkt. Madeni
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Arusha Dkt. Christopher Nzela amesema kuwa chama hicho kimejitolea vifaa hivyo ikiwa ni kuiunga mkono Serikali ya awamu ya Tano katika kuboresha huduma za jamii na wanaahidi kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya kuboresha huduma za afya Jijini Arusha.
“Ni wajibu wetu kama wasaidizi wa Serikali wakati wa maafa tunashughulika na maafa na wakati wa amani tunajikita katika masuala ya afya, elimu na vitu vingine kwa ajili ya ustawi wa wananchi na nchi kwa ujumla ” Alisema Dkt, Nzela
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na magodoro 10,blanket 7, pampu 2 za kupulizia dawa, viatu vya mvua pea mbili , ndoo mbili za kunawia mikono zenye ujazo wa lita 20 kila moja, vyombo viwili vya kuhifadhia taka, madumu matano ya kuhifadhia maji na madiaba mwawili ya kunawia mikono yenye ujazo wa lita 50 kila moja vyenye yhamani ya shilingi 876,0000/= za Kitanzania.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa