Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni amewatakia kheri wanafunzi wa shule za Msingi jiji la Arusha wanaotarajia kufanya mitihani ya kumaliza elimu yao ya shule ya msingi Tarehe 05 na 06/09/2018 katika shule mbalimbali zilizoko Jijini hapa.
Akizungumza Ofisini kwake Dr. Madeni amesema idadi ya Watahiniwa wa Darasa la Saba watakaofanya mitihani katika siku hizo ni 10715 ambapo kati yao Wavulana ni 5178 na wasichana 5537.
“Naamini walimu wa shule za msingi katika Jiji hili wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wetu wanafanya vizuri katika masomo yao na kuongeza ufaulu katika mitihani, hivyo nichukue fursa hii kuwatakia kila la kheri wanafunzi wote mnaotarajia kufanya mitihani yenu ya kumaliza Elimu ya Msingi" aliongeza Dr. Madeni.
Naye Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Bi. Eunice Tondi amesema kuwa vituo vya kufanyia mitihani ni 124 na wanafunzi wataanza kufanya mitihani pasipo kuwa na changamoto yoyote.
"Mitihani itanzaa vizuri na hadi sasa hakuna changamoto yoyote kubwa iliyojitokeza " alisema Bi. Tondi.
Ameongeza kuwa anaamini wanafunzi watafanya vizuri kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu wao na wao wamefanya mazoezi ya kutosha.
Mtihani wa Taifa wa Darasa la saba unahusisha shule mbalimbali za msingi nchini kote zikiwemo za Serikali na za binafsi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa