Katika kuhamasisha Utalii wa ndani na wa nje Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni amedhamini Safari ya kitalii kwa Washiriki wa Mashindano ya urembo ya Miss Journalism World 2018 kutoka Mataifa 13 duniani kutembelea hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Dkt. Madeni amesema kuwa utalii ni chanzo kimoja wapo kikubwa kinachochangia pato la serikali na fedha za kigeni hivyo kila mtanzania kwa nafasi yake anapaswa kuzipa kipaumbele shughuli za kitalii na kuenzi tamaduni zetu.
........................................................................................................................................................................................................................
Miss Journalism World 2018 ni shindano jipya lililobuniwa kwa mara ya kwanza barani Afrika na kijana wa kitanzania Bw. Samwel Chazi na pia ni shindano la 7 kwa ukubwa Duniani katika tasnia ya urembo.
lengo kuu la mashindano haya ni kutangaza vivutio vya utalii kimataifa hasa Bonde la Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Olduvai gorge pamoja na kutangaza utalii wa kitamaduni katika nchi yetu
Kilele cha mashindano hayo kinatarajiwa kuwa kesho Tarehe 15/12/2O18 katika ukumbi wa Mount Meru Hotel ambapo atakayeibuka mshindi katika mashindano hayo atapata fursa ya Kuwa balozi wa kimataifa wa Mlima Kilimanjaro na atakuwa na majukumu ya kutangaza Mlima Kilimanjaro duniani kote.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa