Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Juma Hamsini amesema mbali na halmashauri hiyo kutenga fedha za za miradi ya maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha halmashauri imepanga kutenga kiasi cha fedha Milioni 20 kwa mwaka 2024/2025kwa ajili yakusaidia watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo, alipokuwa akipokea viti vya mwendo kasi 10 kutoka kwa taasisi ya Conservation Foundation Tanzania.
Juma Hamsini amesema, kutokana na uhitaji wa vitu hivyo kwa watu mbalimbali uliobainishwa na idara ya maendeleo ya jamii ikiwemo kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya na watu mbalimbali walioomba kusaidiwa.
Aidha,ameitaka jamii kuwakubali watu wenye ulemavu, ili mahitaji yao yaweze kuibuliwa na kupatikana kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasis ya Conservation Foundation Tanzania Rose Bekker amesema taasis yake imetoa jumla ya viti 10 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5.
Amesisitiza kuwa taasis yake itaendelea kushirikiana na Serikali hususani katika kusaidia watu wenye uhitaji wa viti mwendo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa