Halmashauri ya Jijila Arusha leo Tarehe 07/05/2020 imetia saini mkataba mdogo (Addendum No.3) na kampuni ya SINOHYDRO CORPORATION LTD kutoka China ikiwa ni kazi ya nyongeza ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Oljoro Murriet yenye urefu wa kilomita 2.6
Mradi huu wa ujenzi wa barabara ya Oljoro Murriet utaenda sambamba na ujenzi wa uzio kwaajili ya kuongoza wanafunzi kuvuka barabara katika sehemu mahsusi kwa shule za msingi Osunyai, Sombetini, Mwangaza na Ngarenaro. Ujenzi wa jukwaa la uwanja wa kisasa wa michezo shule ya msingi Ngarenaro, ununuzi na ufungaji wa mashine ya kuchakata taka katika dampo la kisasa lilopo mtaa wa Murriet kata ya Sokon I pamoja na ufungaji wa pampu za maji safi na maji taka katika dampo hilo.
Mradi wa Oljoro Murriet na shughuli zingine zitakazoambatana nao utagharimu kiasi cha fedha za kitanzania Bilioni 6.06 hadi kukamilika ukiwa chini ya TANZANIASTRATEGIC CITIES PROJECT (TSCP)- AF2 ambapo unahitajika kukamilika ndani ya mwezimmoja na siku 15 ikiwa ni kuanzia 11 Aprili 2020 hadi 26 Mei 2020.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa