Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid.S.Madeni amesema upo umuhimu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kushirikiana na sekta mbalimbali za Serikali na na zisizo za Serikali ili kuleta chachu katika kuinua uchumi wa Jiji la Arusha pamoja na kupanga mikakati ya kuboresha mazingira ili kuwavutia wawekezaji, wafanyabiashara na watalii wa ndani na nje ya nchi katika Jiji la Arusha. mkoa wa Arusha, Tanga, Mbeya na Mtwara.
Ametoa maagizo hayo leo katika mkutano uliohudhuriwa na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zikiwemo AUWSA, NEMC, TANROADS, TANESCO, SIDO, na NIRAS pamoja na kamati ya fedha na utawala ya Jiji la Arusha uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuratibiwa na Benki ya dunia kwa lengo la kutengeneza mkakati wa maendeleo ya ukuaji wa uchumi kwenye mikoa minne Arusha, Tanga, Mbeya, na Mtwara ili kuleta mkakati ambao utatumika na mikoa hiyo minne na hata mingine.
Pia Dkt. Madeni alisema kuwa Halmashauri nyingi nchini zina changamoto ya vyanzo vya mapato hivyo ni vyema kujenga mikakati ya pamoja ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza hayo alitoa mfano wa sekta ya utalii Jiji la Arusha kuwa naukosefu wa watu wenye ueledi wa kuongea na kuwavutia watalii hivyo ni vema kuangalia ni mikakati gani itakayo wafanya watalii wakae kwa mda mrefu katika Jiji la Arusha hii ikiwa ni pamoja na kujenga maeneo maalum yenye vivutio vya kitalii ili kupelekea watalii wanapokuja Arusha isiwe tu kama sehemu ya kupita bali Jiji likawe nikivutio kimojawapo.
Mwakilishi wa kampuni ya NIRAS Bw. Ndg. Larry Abermann amesema kuwa wamekuja na mapendekezo na mikakati itakayo tumika na Jiji la Arusha kwa maendeleo ya Jiji, alishauri kuwatengenezea uelewa wa ndani zaidi wakazi wa Jiji la Arusha kuhusu suala la usafi wa mazingira nakusema kuwa Jiji la Arusha lina fursa za kitalii hivyo ni muhimu kuhamasisha usafi wa mazingira na kuangalia namna ya kuweka kitengo maalumu cha kusimamia swala hilo. Naye mkurugenzi wa NEMC Ndg. Aleise Nzari alisema kuwa ni vyema kuchukua mazingira yanayotuzunguka kama fursa kwani Jiji la Arusha lina bahati ya kuwa na hoteli nyingi ambazo zikitumiwa vyema ni njia ya kutangaza utalii na utamaduni wetu kamavile kutenga maeneo rasmi ambayo yatatumika kuuza bidhaa za kitalii pamoja na vyakula vya asili ya makabila na nchi mbalimbali.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa