Halmashauri ya Jiji la Arusha imepata asilimia 96.6 za utoaji fedha za lishe kwa mwaka 2023/2024.
Zoezi la utoaji fedha linafanyika kwa kila robo ya mwaka kwa kila mtoto chini ya miaka 5 kupatiwa shilingi 1000.
Akizungumza katika kikao cha robo ya nne kwa mwaka 2023/2024 Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Shabani Manyama amesema kiwango hicho kimeongezeka ukilinganisha na kile cha mwaka jana 2022/2023 kilikuwa asilimia 67.8.
Amesema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 28.8,amempongeza Afisa lishe Bi. Namsifu kwa juhudi hizo zakuhakikisha fedha za lishe zinawafikiwa walengwa.
Bwana Manyama amesema, katika Jiji la Arusha utoaji wa chakula mashuleni umeongezeka katika shule za kata mbalimbali na hivyo kuwawezesha wanafunzi wengi kupata chakula Shuleni.
Kwa upande wake, Afisa Lishe Jiji la Arusha Bi. Namsifu Godson amesema kuna baadhi ya shule wazazi wamekuwa wazito kuchangia fedha za chakula kwa Watoto wao, hii imesababisha Watoto hao kukosa chakula cha mchana.
Katika kuhakikisha Watoto wote wa shule za Jiji la Arusha wanapata chakula Shuleni, Halmashauri inaendelea kuwahamasisha wazazi kupitia bodi za shule kwa kuwapa elimu ya umuhimu wa Watoto kula shule ikiwemo ongezeko la ufaulu kwa Watoto hao.
Kikao cha lishe robo ya nne kwa mwaka 2023/2024 kimejumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini na asasi za kiraia.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa