Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya Amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kujiandikisha kwenye maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura.
Amesisitiza hayo alipokuwa akizungumza kwenye kikao baina ya viongozi wa kata, mitaa na wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
"Kujiandikisha kwenye maboresho ya daftari la kupiga kura kutatoa nafasi kwa kila aliyejiandisha kupiga kura kipindi cha uchaguzi",alisema.
Amewataka viongozi hao wa ngazi ya kata na mitaa kuwahamasisha wananchi wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Mwenyekiti huyo yupo katika ziara ya kata kwa kata katika Wilaya ya Arusha kwa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa