Na Mwandishi Wetu,
Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mwenyekiti wa Mawaziri wanaoshughulikia maswala ya Serikali za Mitaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALGA) Mhe. Innocent Bashungwa amesaini makubaliano na Sekretariati ya Jumuiya hiyo ili kuweza kuboresha ushirikiano kwa lengo la kufufua uchumi kwa nchi za Jumuiya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baaya ya kufunga mkutano wa siku tatu uliokuwa unaendelea Jijini Arusha, Mhe Bashungwa amesema makubaliano hayo yamezingatia vipaumbele pamoja na hatua za kimkakati za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa uchumi wa EAC ambapo chini ya Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan tumeweza kufikia hatua hii ambayo kwa kipindi cha miaka kumi haikuwahi kufikiwa” alisema Mhe.Bashungwa.
Aidha, amesema kupitia muongozo na maelekezo ya Mhe.Rais samia Suluhu Hassan, serikali inaendela na jitihada ya kupeleka huduma kwa wannchi hasa waishio vijijinikupitia TAMISEMI, na kwamba huduma kwa wateja ndani ya ofisi ya Rais TAMISEMI imekupunguza adha ya wananchi waliokuwa wanaende Wizarani kufuata huduma hizo.
Naye Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amesema, serikali ya Tanzania inaendelea kuhakikisha wanaboresha maendeleo ya serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na kupeleka fedha katika kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kama vile shule, hospitali, barabara, maji na miundombinu mbalimbali.
Katika kuhakikisha kuwa makundi maalumu nayo yanapewa kipaumbele ili kuwainua kiuchumi, Pro. Shemdoe amesema kila halmashauri nchini inatoa aslimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa makundi maalumu ya watu wenye umelavu, vijana pamoja na wanawake sanjari na kutengeneza ajira kwa kwa wakandarsi wadogowadogo pamoja na mafundi wa mtaani kwa kuwapa kazi kwenye ujenzi wa miradi ya serikali za mitaa kama vile shule na hospitali.
“Mpaka kufikia mwezi Januari mwaka huu wamejenga zaidi ya shule elfu 50 bila kuajiri mafundi kutoka nje kwakutumia mafundi wanaopatikana katika maeneo husika ,hivyo wametoa ajira kwa wazawa na kuongeza kuwa atahakikisha fedha zote zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya serikali za mitaa zinawafikia walengwa” Alisema Fro. Shemdoe.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki Getruda Rose Gamwera Aijuka, amesema atahakikisha kuwa jumuiya hiyo inakuwa sehemu za kukutanisha watu wa sekta mbalimbali na kuwa sehemu ya kufanya soko huria ndani ya nchi hizo pamoja na kuboresha mazingira na kuhakikisha sekta binafsi na sekta nyingine zinajumuika katika kuboresha maendeleo ya serikali za mitaa katika nchi zote.
Naye Innocent Uwimana,Rais wa RALGA na Mwenyekiti wa EALGA, amesema atahakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana na jumuiya ya afrika mashariki ili kuhakikisha kwamba sekta ya serikali za mitaa katika jamii ya afrika mashariki inakua na kutoa kipaumbele katika serikali za mitaa za nchi ya jumuiya ya frika mashariki.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa