Na Mwandishi Wetu
Arusha
Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM katika Wilaya ya Arusha Mjini imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Jijini Arusha.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Wilaya ya Arusha Dkt. Wilfred Ole Mollel alisema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuhakikisha ilani ya chama hicho imetekelezwa vizuri.
"Ninashukuru miradi yote ambayo tumeikagua inaridhisha kwa Kiasi kikubwa Sana nimpongeze mkuu wa Wilaya niwapongeze pia Wataalamu wa Jiji kwa kujinasua kutika kusemwa vibaya hasa katika Suala la utumiaji wa pesa nyingi Sana ukilinganisha na kazi zilizofanyika kwa kweli zilikiwa hazirandani lakini sasa hivi nimeridhika na kazi iliyofanyika vizuri sana tena kwa ubora wa hali ya juu sana" alisema Dkt. Mollel.
Pia, Dkt. Mollel alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa pamoja na viongozi na watumishi wote wa Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kuielewa Serikali na kuitendea haki katika miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa watahakikisha kila baada ya mwezi mmoja wanafanya kaguzi za kustukiza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa aliishukuru kamati ya siasa ya wilaya ya Arusha kwa kutembelea miradi hiyo ya maendeleo.
"Na kama tulivyokuwa tunasema siku zote jicho letu halioni tunavyokuwa na macho mawili tunaona kwa msukumo huu ambao tumekuwa nao tumeona kweli vitu vinaenda na sisi tuwaahidi tutaendelea kusimamia miradi yote ya Halmashauri iwe na thamani ya fedha lakini iwe na ubora unaoridhisha " alisema DC Mtahengerwa.
Aidha miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa shule mpya ya Msingi Korongoni uliopo Kata ya Lemara, Ujenzi wa jengo jumuifu la wagonjwa wa nje (OPD Complex) katika hospitali ya Jiji Kata ya Engutoto, Ujenzi wa barabara ya Themi - Viwandani yenye urefu wa 1.4km kwa kiwango cha lami, Ujenzi wa jengo la kutolea huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) zahanati ya Olkereyan Kata ya Moshono na miradi mingineyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa