KamatiI ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Arusha imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe wengine, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Naibu Meya Mhe. Abraham Mollel amesema kwa sasa miradi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha inaonekana.
Amesema, juhudi hizo zakutekeleza miradi hiyo imetokana na ushirikiano uliopo kati ya wataalamu ,Baraza la Madiwani na Viongozi wa Wilaya.
Vile vile, amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imeweza kukusanya mapato kwa asilimia 91.
Amesisitiza zaidi kuwa, Halmashauri kupitia Kamati hiyo ya fedha imeweza kutumia fedha zaidi ya Bilioni 11 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati ya fedha ya Halmashauri ya Jiji la Arusha imefanya ziara yake ya kawaida ya robo ya nne ya mwaka 2023/2024 ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika Jiji hilo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa