KAMATI YA MIPANGOMIJI YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe.Jacob Mollel amempongeza mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Njiro Bi Furaha Kasanda kwa kusimamia ukarabati wa Madarasa 19 katika shule hiyo.
Amesema, uzalendo aliouwonesha mwalimu huyo ni Mkubwa sana kwa kukarabati Madarasa 19 kati ya 8 aliyoletewa fedha.
Akisoma taarifa ya ukarabati wa Madarasa hayo Mwalimu Furaha amesema alipatiwa fedha kiasi cha milioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa Madarasa 19 na mradi upo hatua za ukamilishaji.
Wakati huo huo Mhe. Mollel amemtaka Mkarasi anaejenga jengo la utawala M/s Tribe Construction Limited JV Tanzania Building Works kuhakikisha anakabizi jengo hilo ndani ya muda aliopangiwa.
Jengo hilo la Utawala litagharimu kiasi cha Bilioni 11 hadi kukamilika kwake.
Kamati ya Mipangomiji Jiji la Arusha imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa