Na Mwandishi wetu
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha imefurahishwa na utekelezaji wa Mradi wa Hospitali ya Jiji la Arusha ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia watalii wanaokuja kutembelea Vivutio vya kitalii Mkoa wa Arusha na nje ya Mkoa Arusha .
Hospitali hiyo ambayo imeanza kuhudumia wagonjwa itakuwa na uwezo wa kutua ndege juu ya paa la Hospitali nakumshusha mgonjwa aweze kupatiwa matibabu badala ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Bw, Zelothe Steven akizungumza kwa niaba ya Viongozi wenzake wa CCM alioambatana nao alisema kuwa wamefurahishwa na mradi huo na kwamba kukamilika kwa Hospitali hiyo kutaondoa adha ya watu hususani watalii kwenda kutibiwa nje ya Jiji la Arusha.
Amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwamba kitendo cha kuibua Mradi huo wa Hospitali imeonyesha ubunifu na upeo mkubwa wa maendeleo na nia njema yakuleta mapinduzi ya maendeleo katika Jiji la Arusha.
"Mimi nikiwa kama Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi niwapongeze kwa sababu naona maono yenu yana tija, lakini pia mnafikiria kwa mapana zaidi hasa katika utekelezaji wa Ujenzi wa mradi huu" alisema Zelothe.
Anawataka kuhakikisha Mradi huo unakamilika kwa wakati pamoja nakuendelea kusimamia kwa uadilifu
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk. John Pima ameishukuru Kamati hiyo ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kufuatilia utekelezaji wa miradi na kwamba Jiji la Arusha litaendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza miradi kwa ipasavyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa