Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dk.Athuman Kihamia amesema atashirikiana na Viongozi wote wa Mkoa wa Arusha, wadau wa maendeleo na wananchi kwamba Umoja na mshikamano ndiyo silaha pekee ya maendeleo.
Dk.Kihamia akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Viongozi wa Serikali na wadau wa maendeleo waliojitokeza kumpokea alisema kuwa atafanya kazi na kila mtu katika Mkoa wa Arusha.
Alisema kuwa ni kweli katika Mkoa wa Arusha ni mwenyeji na kwamba sababu hiyo inampa fursa kufanya kazi na kila mtu na kudai kuwa nia ya Serikali nikuwaletea wananchi maendeleo kwamba tofauti zisizo na tija ziwekwe pembeni kazi ya maendeleo iendelee.
Awali Mkuu wa Wilaya Arusha Mh. Kenan Kihongosi akimkaribisha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mh. John Mongela alimhakikishia ushirikiano na Umoja na kudai kuwa Viongozi wa Arusha wana Umoja na mshikamano.
Mh. Kihongosi alisema kuwa maendeleo yeyote duniani yanategemea Umoja na mshikamano na kwamba Arusha umoja na mshikamano ni kipaumbele kwa kila mtu kwa sasa.
Katibu Tawala huyo alipokelewa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk.John Pima,Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na viongozi wengine ikiwa ni pamoja na kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha.
PICHANI ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dk.Athuman Kihamia akisalimiana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima wakati Katibu Tawala huyo alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa