Mkurugenzi wa jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia amemaliza mgogoro wa wafanyabiashara wajenzi wa vibanda uliodumu kwa miaka saba bila kutatuliwa katika kata ya Murriet kwenye eneo la Kwamorombo Jijini Arusha.
"Mpaka kumaliza mgogoro huu nimefanya vikao sita, vitatu katika ofisi za halmashauri ya jiji la Arusha na vitatu nilikuja kufanyia hapa katika kata yenu ambavyo vyote vilikuwa na lengo la kumaliza tatizo hili la muda mrefu” alisema Kihamia
“Eneo hili lina zaidi ya vibanda 300 hivyo niwaombe wafanya biashara wote muwe watulivu wakati tunawaandalia mikataba yenu ya miaka 10 mkiwa kama wafanyabishara wajenzi ili baada ya hapo vibanda vyote vitarudi kumilikiwa na halmashauri na mtaendelea kulipa kodi kama wapangaji kwa mujibu wa sheria" alimalizia Mkurugenzi huyo.
Hivi karibuni mkurugenzi Kihamia alitatua mgogoro uliodumu kwa miaka 10 maeneo ya stendi ndogo jijini Arusha ukihusisha wafanyabiashara wapangaji pamoja na wafanyabiashara wajenzi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa