Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athuman Kihamia wakati wa kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa mapema tarehe 11 Oktoba 2017
Kikao hicho cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2017/2018 ulioanza julai mwaka huu kililenga kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana katika Halmashauri ya Jiji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 sambamba na kuweka mikakati madhubuti ya utendaji kazi katika mwaka huu wa fedha uliopo, kujadili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ili wananchi waweze kufaidika na huduma bora itolewayo katika halmashauri ya jiji la Arusha.
Miongoni mwa mambo yaliyosisitizwa na Mkurugenzi Kihamia wakati wa kikao hicho ni pamoja na suala la nidhamu ambapo amewapongeza watumishi wa jiji la Arusha kwa kuwahi kazini na kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia Wananchi.
Aidha katika idara ya Afya suala la TIKA limeimarika, ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya unaendelea .“Kumekuwa na hulka kwa baadhi ya wahudumu katika vituo vya afya kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa hivyo, nitoe onyo waache mara moja na hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watumishi wote watakaokiuka agizo hili “ alisema Kihamia
“Watumishi mnapaswa kutokuwa na nidhamu ya uoga, pale ambapo mambo hayaendi sawa ni lazma tuambizane kwa maslahi ya wananchi wetu tunaowatumikia na Taifa letu kwa ujumla.” Aliongeza Mkurugenzi huyo.
Aidha suala la kubana matumizi alitaka lipewe kipaumbele na watumishi wote wawe na nidhamu ya fedha ili malengo yaliyowekwa katika halmashauri ya jiji la Arusha yaweze kufikiwa kwa kiasi kikubwa.
Pia alipongeza idara mbalimbali zilizofanya vizuri katika mwaka wa fedha uliopita ikiwemo idara ya Bishara kwa ongezeko la 12% ya mapato ya ndani.
Kwa upande wa idara ya Mipango Miji kero za ardhi zinachukuliwa hatua, ujenzi wa barabara mbalimbali unaendelea chini ya wakala TARURA na hivi karibuni kutatolewa leseni za makazi kwa wananchi wote wa jiji la Arusha.
Zaidi ya Bilioni 357 za kitanzania zimetolewa katika mradi wa kunusuru kaya masikini (TASAF) na kuondolewa kwa wafaidika wasiostahili .
Kwa upande wa idara ya utawala, idara imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanikisha kuondolewa kwa waatumishi hewa, watumishi wenye vyeti feki na mishahara hewa.
Idara ya Elimu Msingi zaidi ya Bilioni 18 za kitanzania huwekezwa katika suala la Elimu bila malipo chini ya uratibu wa Bw. Odilo Kalinga ambaye ni mratibu wa elimu bila malipo kwa halmashauri ya jiji l Arusha.
Kupitia kuwepo kwa dawati la malalamiko kero za wananchi zimeshughulikiwa na hali imepelekea malalamiko kupungua.
Katibu wa ccm wilaya ya Arusha Mhe. Mussa Matoroka pia alihudhuria kikao hicho kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na kuhakikisha inatekelezwa kikamilifu.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa