Maadhimisho ya siku ya vijana duniani leo tarehe 10/08/2019 yamefanyika kiwilaya katika viwanja vya General Tyre Jijini Arusha.
Siku ya vijana duniani ni siku ambayo vijana na wadau wanaojihusisha na masuala ya vijana hukutana kutathimini shughuli zilizofanywa kwa vijana na kujadili namna ya kutatuta changamoto zinazowakabili.
Maadhimisho hayo yameambatana na maandamano ya vijana kuanzia makao makuu ya Jiji la Arusha kuelekea uwanjani ambapo vijana walipatiwa mafunzo ya afya na ujasiriamali pamoja na huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi (VVU).
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa .
katika hotuba yake, Ndg. David Mwakiposa aliwahamasisha vijana kujitokeza kuchukua mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani pamoja na kutoa rai ya kutunza afya.
“Taifa haliwezi kuendelea bila vijana wenye nguvu hivyo nichukue fursa hii kuwaasa tutunze afya zetu ili tuweze kuijenga nchi yetu” alisema Ndg. David Mwakiposa.
Kauli Mbiu:
“Kuelekea 2023, Tanzania ya viwanda: kuboresha elimu kwa vijana kwa maendeleo ya taifa”
Pichani: Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani, Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akikagua bidhaa za vijana wajasiriamali
Kulia: Mtaalamu wa kutoa elimu ya ukeketaji na masuala ya uzazi salama kutoka asasi isiyo ya kiserikali HIMD, akitoa elimu kwa vijana
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa