Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dakta. Hassan Abbas alipokuwa akiwamegea Maafisa Habari wa Mkoa pamoja na Jiji la Arusha siri kuu Nne (4) za mafanikio katika kuleta mageuzi katika sekta ya Habari Serikalini.
Ameyasema hayo alipowatembelea Maafisa Habari wa Mkoa pamoja na Jiji la Arusha mapema hapo jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo lengo kuu la ziara hiyo ilikuwa ni kubaini changamoto mbalimbali zinazowakumba maafisa habari hapa nchini.
Siri nyingine tatu ni pamoja na kuwa washauri na wasemaji wakuu washughuli zinazofanyika katika maeneo yao ya kazi, kujali muda pamoja na ushirikiano baina ya maafisa husika.
“Kada ya habari ni muhimili mkubwa wa taifa hili hivyo wanahabari wote katika ngazi ya serikali mnapaswa kuisimamia kada hii kwa weledi na kujituma kwa hali na mali na mtambue nafasi zenu zina mchango mkuwa kwa serikali katika kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi” alisema Dakta. Abbas.
Aliongeza kuwa, kada ya Habari Serikalini iwe chachu ya kusaidia kutangaza na kutetea mageuzi mbalimbali yanayoendelea hapa nchini chini ya serikali ya awamu ya Tano.
Katika zara yake hiyo Dakta. Abbas aliambatana na uongozi mzima wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) ambapo mkakati huo wa idara ya Habari Maelezo na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali ni endelevu katika Mikoa na Halmashauri zote hapa nchini.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa