Maafisa watendaji wa Kata Halmashauri ya Jiji la Arusha wasaini mkataba wa upangaji,ufuatiliaji na utekelezaji wa afua za lishe Tarehe 28 Agosti 2019 ilikufanikisha swala la uboreshaji wa hali ya lishe na kupunguza athari zautapiamlo kwa jamii hasa udumavu.
Mkataba huu ulisainiwa baina ya mwajiri ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji laArusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni na Maafisa watendaji wa Kata ili kuhakikisha kuwa maswala ya lishe yanakuwa agenda ya kudumu katika vikao vya kisheria vya kamati ya maendeleo ya Kata pamoja na kufanikisha utekelezaji wa siku ya afya kwa Kata zote.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bi.Rose Mauya akizungumza na watendaji hao wa Kata amesema Tanzania kiwango cha utapiamlo ni kikubwa ikiwa ni asilimia 34 ya udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 kwa mwaka 2015/2016, hivyo mikakati ya Serikali katika kupambana na utapiamlo kwa kuweka msisitizo wa utekelezaji imeandaa mkataba ambao walisainishwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kisha wakurugenzi wa Halmashauri na watendaji wa Kata.
Maafisa watendaji hao wamesema watahakikisha wanafanyia kazi rasimu ya mkataba huo na kusimamia utekelezaji wake kwenye Mitaa iliyopo katika Kata wanazosimamia.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa