Na Mwandishi Wetu
Arusha
Wilaya ya Arusha imeonyesha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kuongezeka kutoka asilimia 2.8 mwaka 2020 hadi asilimia 3.1 mwaka 2021.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanayofanyika Disemba Mosi kila mwaka, Mkuu wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda amesema Wilaya ya Arusha wanalo jukumu la kuendeleza mipango mizuri ya kukabiliana na ongezeko la UKIMWI.
Pichani: Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani,Disemba Mosi, 2022.
"Kwa jamii na watanzania wanaendelea kupima na kujua afya zao na pale tunapobaini afya zetu ni vyema tufuate utaratibu uliowekwa na serikali na wale ambao wanatumia dawa wito wetu watumie kadri walivyoelekezwa na wataalamu wa afya,"amesema Mtanda.
Aidha amewasisitiza wananchi wa Wilaya ya Arusha wanaotumia dawa kujiepusha na kueneza maambukizi kwa watu wengine kwa makusudi kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Mwakilishi wa watu wanaoishi na VVU Wilaya ya Arusha,Caroline Chami amesema katika wilaya ya Arusha mafanikio yapo ya kupambana na ugonjwa huo ikiwa jitihada zote zinatokana na mshikamano na juhudi za serikali na wadau mbalimbali.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Hargney Chitukuro amesema kuwa wataendelea kutoa huduma za afya na kuziboresha pamoja na kuzisogeza karibu na wananchi ili kila mwananchi aweze kufikiwa na huduma za afya.
"Kwani tunaona takwimu zinazotolewa za asilimia 1.9 ya maambukizi katika mkoa wetu,nina imani kwa huduma hizi zinazotolewa zitazidi kupungua,"amesema Chitukuro.
PICHANI: Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Hargeney Chitukuro akitoa neno katika Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani.
Sambamba na hilo Jiji la Arusha limetoa kadi za Bima ya afya 100 katika kaya 20 ambazo hazina uwezo hivyo wataendelea kuangalia eneo hilo pamoja na kuwasaidia wengine.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa