Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda amezindua vyumba 105 vya madarasa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha tarehe 27/12/2021 kwakuwataka watumishi wa sekta ya elimu kuungana ili kupata mafanikio makubwa.
Tukio hili la kihistoria katika sekta ya elimu lililowakutanisha wadau wa elimu katika Shule ya Sekondari Themi kwaajili ya uzinduzi, Mhe. Mtanda ameeleza kua kuungana kwa watumishi wa sekta ya elimu kutawapa nguvu ya kufanya mambo makubwa na kuleta mafanikio makubwa katika sekta hiyo huku akiwataka watendaji wa serikali kua kitu kimoja ili waweze kuwahudumia wananchi.
“Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu katika sekta ya elimu ili tupate mafanikio makubwa ni lazima tuungane kwa pamoja…watendaji wa Serikali popote walipo, tuwe kitukimoja ili tuwahudumie wananchi” amesema DC Mtanda.
Aidha Mhe. Mtanda Amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SSH kwa kundelea kutatua kero ya uhaba wa madarasa nchini huku akimpongeza mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mkurugenzi wa Jiji, Afisa Elimu Sekondari, Madiwani na Wananchi kwa usimamizi bora uliopelekea kukamilika kwa majengo kwa wakati na Ubora.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmillian Iranqhe ameeleza kua fedha hizo zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa vyumba hivyo zimetumika vizuri huku akilipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kua yakwanza miongoni mwa Halmashauri zote kukamilisha ujenzi huo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima ameeleza kua mwaka ujao wanafunzi waliofaulu wataanza kusoma kwa pamoja kwani kutakua na chaguo moja tu, huku akiwaomba wazazi kujianda na mwaka mpya wa masomo kwa kuwaandaa watoto wao kisaikolojia, kuwanunulia mahitaji muhimu ya shule huku akiwataka walimu kujiweka tayari kwa kazi.
Hatahivyo Afisa Elimu Sekondari Jiji la Arusha Bw. Valentine Makuka ameeleza kua ujio wa vyumba hivi vya madarasa vitapelekea kuongezeka kwa ufaulu na kukua kwa sekta ya elimu kwani katika darasa moja watakaa wanafuzi 50 tu huku wanafunzi wote waliofaulu wakipata nafasi ya kwenda shule kupata elimu.
Jiji la Arusha limepata jumla ya vyumba 105 huku 16 kati ya hivyo vikiwa ni maghorofa na Fedha zilizotumika katika Ujenzi huo zimetokana na mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambapo shule zitakapofunguliwa 17/1/2022 na madrasa hayo yataanza kutumika kufundishia wanafunzi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa