Madiwani ,watendaji wa kata watakiwa kuwa mabalozi wa kuelezea miradi ya serikali ya awamu ya tano kwa wananchi na kuwahimiza kuitunza .
Na Mwandishi wetu
MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na watendaji wa kata katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ,wametakiwa kuwa mabalozi wa kuwaelezea wananchi miradi mikubwa inayotekelezwa na Seriali mojawapo wa mradi huo ukiwa ni mradi wa maji ,Jijini Arusha wenye thamani ya Tshs billion 520 inayotekelezwa na Serikali chini ya uongozi wa Dk.John Pombe Magufuli .
Mradi huo unatekelezwa na kusimimiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha ambapo hadi sasa mradi huo katika Jiji la Arusha umefikia hatua nzuri na kukamilika kwa mradi huo kutaondoa tatizo la maji katika Jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Kenan Kihongosi mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa huduma za maji safi na Usafi wa mazingira Jiji la Arusha anawataka Madiwani na watendaji kuwa mabalozi wa kuelezea mradi huo na kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya tano bila kusita .
Kimsingi alisema kuwa anaona fahari kuona jinsi ilani ya Chama cha mapinduzi inavyotekelezwa na kudai kuwa hayo ni matunda ya uongozi bora na uliotukuka wa Mh. Rais Dk.John Pombe Magufuli
Mh.Kihongosi alisema namna pekee ya kumshukuru Rais Magufuli ni kuelezea wananchi miradi inayotekelezwa chini ya uongozi wake na kuwahimiza kutunza miradi hiyo kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho .
Meya wa Jiji Halmashauri ya Jiji la Arusha Mh. Maxmilillan Matle Iranqhe akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake amedai kufurahishwa na utekelezaji wa mradi wa Tshs Billion 520 na kwamba anaona wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wakiondokana na adha ya maji baada ya mradi kukamilika .
Mh. Iranqhe alishukuru Serikali kwa kutambua adha ya wananchi na kuwezesha mradi huo wenye fedha nyingi ambapo anaomba Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira kuhakikisha wanarudisha miundo mbinu pindi wanapomaliza kukamilisha mradi ili kuwezesha wananchi kupita katika maeneo yao bila adha.
ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA ARUSHA MH. KENAN KIHONGOSI AKIAMBATANA NA MADIWANI WA KATA 25, WATENDAJI WA KATA 25, WATAALAM WA AUWSA NA HALAMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KATIKA ZIARA YA KUKAGUA MRADI WA TSH BILLION 520 NA KUWAJENGEA UELEWA VIONGOZI KUHUSU MRADI HUO.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa