Mafunzo hayo yaliyofanyika jana tarehe 30/05/2019 katika ukumbi wa Makumbusho jijini Arusha yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Gabriel Daqarro na yalijumuisha wajumbe wote wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto katika ngazi ya halmashauri .
Pichani: Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto katika ngazi ya Halmashauri wakishiriki mafunzo kwa mtindo wa Kikundi
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha na katibu ni Afisa Maendeleo ya Jamii na Afisa Ustawi wa Jamii na majukumu ya kamati hiyo ni kuratibu shughuli zinazohusiana na mpango na kuboresha utoaji wa huduma kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.
Pichani: Mtoto Zakta Hassan ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Ngarenaro jijini Arusha na pia ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alipokuwa akiwasilisha mawazo ya wajumbe wengine dhidi ya dhana nzima ya ukatili wakati wa mafunzo hayo
Vikundi kazi katika utekelezaji wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni pamoja na kuimarisha uchumi wa kaya, mila na desturi chanya kwa wanawake na watoto zenye usawa wa kijinsia, mazingira salama, malezi, kuimarisha mahusiano na kuziwezesha familia, utekelezaji na usimamizi wa sheria, utoaji wa huduma kwa waathirika wa ukatili, mazingira salama shuleni na stadi za maisha pamoja na uratibu, ufuatiliaji na tathmini.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa