Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro aongoza zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa vijidudu ikiwa ni lengo kuwakinga abiria na maambukizi ya virusi vya Corona pindi wanapotumia vyombo vya usafiri.
Zoezi hili limezinduliwa leo rasmi kwa mabasi yanayotoka Jiji la Arusha kuelekea mikoa mingine , pamoja na vyombo vingine vya usafiri wa umma vinavyotumika katika safari za ndani ya Jiji la Arusha.
Sambamba na mpango huo wa Jiji, leo Chama cha wasafirishaji abiria (AKIBOA) na wadau wa usafirishaji wametoa vifaa vikiwemo vitakasa mikono pamoja na dawa za kupulizia vyombo vya usafiri vyenye gharama zaidi ya Sh.milioni 10 kusaidia wananchi kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.
Akizungumza mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro amesema operesheni hii ya upulizaji dawa itaendela kwa kushirikiana na wadau ambao tayari wameanza kutoa michago ya kuwezesha zoezi hilo.
Daqarro amewataka wananchi wasiwe na taharuki na hofu pamoja kuzusha maneno ya upotoshaji juu ya ugonjwa huo bali waachie mamlaka husika kutoa taarifa pamoja na elimu.
"Kuna watu wana dhana potofu wanasema Corona haiwezi kuwapata watu weusi hayo ni mawazo potofu kikubwa ni kuchukua tahadhari na kufata maagizo ya wataalamu wetu wa afya" amesema
Naye mganga mkuu wa jiji la Arusha Dr. kheri Kagya amesema kuwa ni vyema wasafirishaji wote wahakikishe abiria wanatumia vitakasa mikono au kusafisha mikono kwa maji tiririka kabla ya kupanda chombo cha usafiri ili wafike salama bila maambukizi ya ugonjwa huo.
Amesema kuwa maeneo ya stendi yanauwezekano mkubwa wa kuambukizana hivyo jukumu kuu ni kunawa mikono na kuepuka misongamano isiyo ya lazima kwani itasaidia kuepukana na janga hilo.
Mwenyekiti wa chama cha usafirishaji mkoa wa Arusha na Kilimanjaro (AKIBOA) Locken Adolf Massawe amesema zoezi la upuliziaji dawa vyombo vya usafirishaji ni endelevu na litahusisha vyombo vya usafiri wa jumuia ambapo bodaboda, magari makubwa na madogo.
" AKIBOA tutaendelea kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya ugonjwa huu"amesema.
Mwisho
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa