Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Marko Pima amewasili katika ofisi za makao makuu ya Halmashauri ya Jiji mara baada ya kuapishwa. Dkt. John Marko Pima amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt. Maulid Suleimani Madeni. Makabidhiano haya yalishuhudiwa na wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa Jiji aliyepita Dkt. Madeni amewashukuru watumishi wa Jiji kwa ushirikiano waliokuwa wakimpatia na kuwaasa waendelee kutoa ushirikiano kwa Mkurugenzi Dkt. John Pima
Pichani: Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima na wakuu wa Idara na Vitengo Jiji la Arusha
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa