"Taasisi binafsi zinazojishughulisha na maswala ya lishe zimetakiwa kufanya kazi bega kwa bega na Serikali hususani kwa kuweka wazi bajeti zao na kazi zao".
Kauli hiyo imesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa alipokuwa akifungua kikao kazi cha mpango wa awali wa lishe kwa mwaka wa fedha 2024/2025,Jijini Arusha.
Amesema Serikali kwa upande wake inaendelea kuhakikisha fedha za lishe hasa utoaji wa shilingi 1000 kwa kila mtoto inatolewa kwa wakati.
Mtahengerwa amesema kwa mwaka 2023/2024 Halmashauri imepanga kutoa kiasi cha shilingi milioni 200 zakusaidia lishe kwa watoto hao.
Hata hivyo, amesema fedha hizo kwa mwaka huo zitatolewa mapema zaidi kabla ya mwaka kuisha ili kusaidia kila mlengwa kupatia huduma hiyo mapema.
Aidha,amesisitiza zaidi kwa kila idara inayohusika na maswala ya lishe kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa wakati.
Akiwasilisha mpango wa awali wa maswala ya lishe Afisa Lishe Jiji la Arusha Namsifu Godson amesema Halmashauri kupitia idara yake ya elimu inaandaa sheria ndogondogo itakayombana mzazi kuchangia chakula shuleni.
Amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wazazi wengi kutochangia chakula kwa watoto wao mashuleni na kupelekea kuwa na watoto dhaifu hasa nyakati za mchana.
Pia, mpango uliopo nikuhakikisha afua zote za lishe zinafanyiwa kazi mapema na kuwawezesha kuondoa hali ya udumavu katika Jiji la Arusha.
Kikao cha mpango wa awali cha maswala ya lishe kilijumuisha sekta mbalimbali kama vile Elimu, Kilimo na Ufugaji.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa