Msinanzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arusha mjini Dkt. John Pima amewaapisha Mawakala 11,311 kutoka vyama mbalimbali vya siasa ambapo mawakala 522 wametakiwa kurekebisha mapufungu yaliyobainika katika barau zao za kuomba uwakala .
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Dkt. Pima alisema kuwa walipokea barua zipatazo 11,833 kutoka vyama 15 vya kisiasa ambavyo ni CUF ,CHADEMA ,CCK ,CCM ,ACT ,UDP, DEMOKRASIA MAKINI ,ADA TADEA ,CHAMA CHA SAUTI YA UMMA,UMDP ,NRA ,AAF ,ADC, UPDP na NCCR -Mageuzi .
Dkt Pima alisema kuwa baadhi ya barua alizopokea alibaini mapungufu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kuonyesha majina ya kata na vituo ambavyo mawakala hao watasimamia uchaguzi
Mengine ni Mawakala hao kutokuwa na utambulisho wa katibu kutoka katika chama husika ,kutumika kwa mihuri tofauti katika barua zilitoka chama kimoja ikiwa ni pamoja na mawakala husika kutambulishwa na katibu wa Jimbo badala ya katibu wa Wilaya .
“Kulikuwa na mapungufu na changamoto nyingine ndogondogo ambapo tumeita vyama vyote na kuwaeleza mapungufu hayo na vyama vingi vilifanikiwa kufanya marekebisho na wengine tuliwapa muda wa kurekebisha ili kukidhi vigezo “alisema Dkt.Pima
Alisema kuwa Jimbo la Arusha mjini limefanikiwa kuteua na kuapisha mawakala kutoka vyama vyote 15 vinavyotarajiwa kushiriki uchaguzi mkuu oktoba 28.
Dkt .Pima alitoa wito kwa Mawakala wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi kama sheria ,kanuni ,miiko ,maadili na taratibu nzima za uchaguzi .
Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi wa Jimbo la Arusha kuwa mstari wa mbele kulinda amani na utulivu ili kuwezesha kila mtu kupiga kura bila bughuza
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa