Mwandishi Wetu
Arusha.
Msitahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmillian Matle Iranqhe amekubali kuwa mlezi wa Chama cha Umoja wa Wazee Jiji la Arusha ambapo pia aliweza kutoa milioni Moja ili kuinua mfuko wa wazee.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Tembo Club jijini Arusha amesema kuwa wazee ni Tunu katika Taifa lolote ambapo ameahidi kushirikiana nao Ili kuwapatia dira na wazee wajue wako mikono salama.
Meya Iranqhe alisema kuwa Jiji la Arusha limejipanga ipasavyo kwani zipo huduma nyingi za wazee pia zimetolewa ikiwemo changamoto ya ukosefu wa vifaa vya ofisi ambayo tayari ilishatatuliwa.
Zaidi ya milioni 100 zimetumika Kwa ajili ya matibabu ya wazee jijini Arusha pia zaidi ya milioni 30 imetengwa Kwa ajili ya kuwapatia wazee bima.
Alisema lengo ni kuhakikisha wazee wanakuwa salama kwani ndani ya wazee wapo watu wenye taaluma mbalimbali hivyo yeye kama meya anadhamini vitu vilivyopo ndani yao.
Meya alisema kuwa wazee pamoja na uzee wanapaswa kuendelea kufanya kazi sambamba na mazoezi angalau hata kutembea kilometa 4 Hadi 5 hii inasaidia akili kufikiri sawasawa.
Alisema kuwa miongoni mwa wazee wana uwezo na wanamiliki majumba ambayo ni kama fursa kufuatia kwasasa Jiji la Arusha kupokea watalii wengi sana Huku lengo la Serikali likiwa ni kupokea watalii zaidi ya milioni 5 hii itasababisha hotel kujaa na ikiwa Kuna Mzee ana nyumba pia anweza kujipatia kipato ikiwa atweza kuikarabati ikaka sawa atweza kulaza watalii.
Aliwatia moyo wazee kukataa uzee kama ambavyo wanamkataa shetani na kukimbia vivyo hivyo wajitahidi kupambana na ni lazima mambo yao yatakuwa mazuri.
Katibu wa chama cha umoja wa wazee Jiji la Arusha (UWAJIA) Jiji la Arusha Salim Mvungi amesema kuwa changamoto kubwa zinazowakabili wazee ni chakula,afya,na makazi sambamba na wazee wengi kutajwa kuharibu maadili Kwa jamii vikiwemo vitendo vya ulawiti Kwa watoto,kuwapa watoto mimba, jambo ambalo linaathiri Taifa ikiwa hawatakemewa.
Aliiomba Kila Halmashauri kutenga asilimia 2 au 3 katika mfuko wa Halmashauri Kwa majiji yote Ili kuwasaidia wazee kwani wametumika katika serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii Jiji la Arusha, Isaya Doita ambaye pia ni diwani wa kata ya Ngarenaro amesema kuwa kutokana malalamiko ya dirisha la wazee kwenye vituo vya afya kutopewa kipaumbele ametoa agizo Sasa kuhakikisha wazee wanapatiwa huduma muhimu na kusikilizwa Kwa wakati.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa