Na Mwandishi Wetu
Arusha
Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Viongozi wa Jiji la Arusha kwa kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vya elimu wamefanya usafi katika soko la Kilombero na Stendi ndogo ya Jiji ambapo sasa usafi wa pamoja wa makundi mbalimbali utakuwa unafanyika kila Jumamosi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximillian Iranqhe amesema katika kuadhimisha siku hiyo madiwani wa hilo wameweza kufanya usafi wa mazingira ili kuhamasisha wananchi kuendelea kuweka mazingira safi na salama kwa afya ya viumbe hai.
Aidha amesema kuwa ni takribani miezi sita hali ya Jiji hilo sio safi kutokana na kulegalega kwa usimamizi wa viongozi wa jiji hilo ikiwemo Mwenyeti wa kamati ya usafi na mazingira.
"Kuanzia leo na kuendelea zoezi hili la usafi liendelee ili kuonyesha mfano kwa wananchi Jiji likae safi,"amesema
Isaya Doita ni mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii katika Halmashauri ya jiji la Arusha na ambaye pia ni Diwani wa Ngarenaro amewataka Maafisa afya wa Halmashauri ya Jiji hilo kusimamia zoezi kikamilifu ili liweze kuwa endelevu.
Nao wanafunzi wa vyuo walioshiriki kufanya usafi wanatoa rai kwa wasomi na wananchi kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa