Miradi Wilaya ya Arusha yavunja rekodi, yamfurahisha mkimbiza Mwenge.
Na Mwandishi wetu
KIONGOZI wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi amesema kuwa miradi 11 ya Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha aliyokagua na kuitembelea akiwa na wakimbiza Mwenge Kitaifa ni ya viwango vinavyotakiwa na inauhalisia wa fedha zilizotumika.
Miradi hiyo inathamani ya Tshs 554,605,185,578 ambapo fedha kutoka Serikali kuu ni Tshs 552,250,660,184. Halmashauri Tshs 2,124,047,393, Uwekezaji wa ndani Tshs 228,978,000.00, Nguvu ya Wananchi Tshs 1,500,000.
Luteni Mwambashi akizingumza na wananchi katika Viwanja vya Soko la Kilombero alisema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa miradi katika Wilaya ya Arusha iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge anavunja ukimya na kuelezea mradi wa kiwanda cha kuzalisha matofali ulionzishwa na kutekelezwa na Jiji la Arusha kwamba mradi huo ni wa viwango na Halmashauri nyingine zinapaswa kuja kuiga Jiji la Arusha namna miradi kama hiyo inavyotekelezwa .
Alisema kuwa mradi huo utaleta manufaa kwa kuwa utaongeza mapato ya Halmashauri na kutoa ajira na kwamba fedha zilitumika kutekeleza mradi huo hazina mashaka kwa kuwa zina uhalisia.
Mradi huo wa Matofali umetumia Tshs 93,805,000 ambapo mtambo umenunuliwa kwa Tshs 61,200,000 ,gharama za usimikaji wa mtambo Tshs 13,699,500,ujenzi wa ofisi na stoo Tshs 18,905,500.
Pamoja na mambo mengine alieleza kufurahishwa na miradi mingine ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwemo miradi ya Ujenzi wa madarasa na kutaka Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuendelea kutekeleza miradi kwa viwango vinavyotakiwa kama ilivyo kwa miradi mingine.
Kimsingi alisema kuwa miradi inayoanzishwa ni kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi kwamba inatakiwa kutekelezwa katika viwango vinavyotakiwa
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa