Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Ole Sabaya, wamepongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Arusha.
Pongezi hizo wamezitoa wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Sekei kata ya Sekei jiji la Arusha, mradi ambao umetekelezwa kwa gharama zaidi ya shilingi milioni 584, fedha kutoka Serikali Kuu, kupitia mradi wa kuboresha mindombinu ya shule za sekondari SEQUIP.
Kamati hiyo, Wajumbe hao kwa pamoja wameupongeza uongozi wa halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kukamilisha ujenzi wa shule hiyo kwa wakati na hatimaye wanafunzi 95 waliopangiwa kuanza kidato cha kwanza wakiwa darasani, huku mradi huo ukiwa na viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Mwenyekiti wa UWT CCM mkoa wa Arusha, Florah Zelothe, amewapongeza kwa usimamizi imara wa fedha za umma na hatimaye kukamilisha mradi kwa kipindi kifupi, mradi ambao thamani ya pesa na ubora wa mradi vinaonekana kwa macho na kuwa na mindombinu ya kisasa.
Aidha, wamewataka walimu, kuwasimamia wanafunzi ili kuitunza miundombinu na samani zake ili zidumu kwa muda mrefu pamoja na kutunza mazingira ya nje kwa kupanda miti, kuzunguka eneo lote la shule.
Awali, akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule ya Sekondari Sekei Mwl. Joshua Kisivan Mollel amasema, mradi huo umetumia shilingi milioni 584.2 ukijumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba nane vya madarasa, maabara tatu za masomo ya Sayansi ikiwemo Kemia,Biolojia na Fizikia, Maktaba, jengo la TEHAMA, pamoja na matundu nane ya vyoo vya wasichana na wavulana.
Amesema, Shule hiyo imesajiliwa kwa namba ya usajili S.6448 na tayari imepokea wanafunzi 96 wa kike 50 na wa kiume 46 na ufundishaji umeanza tangu Januari 08, 2024 kufuatia ratiba ya mwaka wa masomo ulioanza 2024.
Kamati ya Siasa Mkoa ilikagua miradi ya sekta ya Elimu na Afya huku ikiridhika na utekelezaji wa miradi unaoendana na thamani ya fedha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa