Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema miradi ya kupunguza umaskini Tanzania (TASAF) kushirikisha wanajamii husika ili wao wasema ni nini wanahitaji.
Maelekezo hayo, ameyasema alipokuwa akifungua kikao kazi cha kujenga uelewa kwa viongozi wa Wilaya ya Arusha na wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mtahengerwa amesema, kupitia kikao kazi hicho Elimu itakayotolewa iweze kushushwa ngazi za chini ili nao waweze kuwa na uelewa wa pamoja katika kutekeleza miradi ya TASAF.
Akitoa taarifa ya miradi, mratibu wa TASAF Mkoa Richard Nkini amesema Wilaya ya Arusha kwa miaka 3 kuanzia 2022 hadi 2024 ilipokea fedha Bilioni 4.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na walengwa.
Amesema, katika miaka hiyo 3 TASAF katika Wilaya hiyo imetoa fedha Bilioni 1.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 26 katika sekta ya Afya na Elimu.
Vilevile, TASAF imetoka kiasi cha Bilioni 2.8 za kupunguza umaskini katika kaya 4,864 na miradi 4 imeweza kutoa ajira za muda.
Nkini amesema, kukamilika kwa miradi ya TASAF kumesaidia huduma za afya kusogezwa karibu na wananchi.
Pia, miradi imewasaidia Kinamama na Watoto kuhudhuria Kliniki na hivyo kupata ushauri bora wa kitaalamu.
Amesema, faida nyingine ni kuboreshwa kwa miundombinu ya Elimu na Afya na pia kutengeneza ajira za muda kwa wananchi.
Nae,Mkurugenzi wa miradi kutoka TASAF Paulo Kijazi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, amesema miradi ya TASAF iliyobaki imalizike katika ubora na kuweza kutoa nafasi yakupata mradi mwingine.
Kikao kazi cha TASAF kilijumuisha viongozi wa Wilaya, Wataalamu wa TASAF kutoka makao makuu na Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa