Na Mwandishi Wetu
Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Injinia Richard Ruyango amemshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutoa Zaidi ya Shilingi milioni 900 kwaajili ya ujenzi wa Madarasa.
Mhe. Ruyango alitoa shukrani hizo leo Tarehe 09, Disemba 2022 Jijini Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella katika mdahalo wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa miaka 61 lililofanyika Chuo Cha Ufundi Arusha(Arusha Technical College) na kushirikiana viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, Wananchi pamoja na wanafunzi wa chuo cha ATC.
Alisema utoaji wa fedha hizo unawezesha mabweni kujengwa ili kuondoa mkimbizano wa ujenzi wa mabweni na madarasa.
Alipongeza Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kuwezesha wananchi kupata matibabu bure katika hospitali ya Mount Meru na kuongeza mafanikio katika sekta mbalimbali.
Aliwapongeza viongozi wa dini kwa kuhubiri masuala ya amani ikiwemo kuliombea Taifa katika kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani.
Naye mzee Emmanuel Munga alitoa rai kwa vijana kutunza amani na kujua historia ya nchi na lazima wajue uzeeni ni hazina na ni tunu ya taifa na kuongeza kuwa historia ni muhimu.
Huku mzee Nyanda alisema wakati wa uhuru mwaka 1961 alikuwa darasa la nne na kuipongeza serikali kwa kuondoa kodi ya kichwa ilikuwa ikiwafanya wananchi kukimbia
Aidha, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Musa Chacha alitoa rai kwa watanzania kulipa kodi ili kuwezesha miradi mbalimbali kutekelezwa na kuishukuru serikali kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa mabweni.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Hargeney Chitukuro alisema alisema hivi sasa Jiji la Arusha lina shule za msingi 168 zikiwemo za serikali na taasisi binafsi, sekondari lakini pia akigusia Jiji hilo kuwa safi sanjari na dampo la kisasa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa