|
Mkurugenzi ,Mkuu wa Wilaya waongoza zoezi la Ujenzi vyumba vya madarasa . Na mwandishi wetu Mkuu wa Wilaya ya Arusha akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wameongoza zoezi la Ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Moivaro Viongozi hao wakizungumzia zoezi hilo wamesifu Wananchi wa Jiji la Arusha na vijana waliojitokeza kushiriki zoezi hilo la kujitolea na kwamba umoja na nguvu ya pamoja itawezesha Ujenzi wa madarasa kwa wakati na kuwezesha wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza bila kikwazo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima anasema zoezi la Wananchi na vijana wazalendo la kujitolea kujenga shule za Sekondari za Jiji la Arusha titaokoa zaidi ya Tshs million 800 ambazo angelipwa mkandarasi katika Ujenzi wa vyumba vya madarasa . Kimsingi alisema kuwa Wananchi wa Jiji la Arusha wanaunga jitihada za Mh m Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuwaletea wananchi wake maendeleo bila kutegemea wafadhili . Alisema kuwa Ujenzi huo utaendelea katika shule nyingine za Jiji la Arusha ambazo ni Sekondari ya Elerai ,Terrat ,Ungalimited . Aliongeza kuwa shule ya sekondari Ungalimited ni shule Mpya inayoanzishwa kwamba anapongeza jitihada za Mbunge wa Jimbo la Arusha za kufanya jitihada kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na kupata baadhi ya vifaa vya Ujenzi katika kata ya Ungalimited . Mh.Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi wakizungumzia zoezi hilo alisifu Wananchi ,vijana walijitokeza katika zoezi hilo na kudai kuwa moyo na nia walionyesha ni ya kizalendo . Alisema kuwa inatia moyo kuna jitihada za Rais Dk.John Magufuli zinaungwa Mkono kwa vitendo na kuwataka Wananchi kuendelea kujitokeza kusaidiana na mafundi katika shule zenye Ujenzi . Pamoja na mambo mengine alisema kuwa kwa umoja na nia ya dhati ya uongozi wa Jiji la Arusha agizo la Waziri mkuu litatekelezwa kwa wakati .
|
|
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa