Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia amefanya ziara ya kutwa nzima kutembelea na kukagua thamani ya fedha katika miradi ya Afya inayoendelea kutekelezwa Jijini hapa.
Miradi aliyoitembelea ni pamoja na mtaro wa kusafirisha maji machafu wenye urefu wa km 1.2, mradi wa dampo la kisasa lililopo Murieti uliopo katika hatua za ukamilishwaji, Kituo cha afya cha Murriet ambacho kipo katika hatua ya upauaji, kituo cha polisi na nyumba za askari Murriet, Kituo cha afya cha Moshono ambacho kimeezekwa bati hivi karibuni pamoja na ujenzi wa zahanati ya Olmot ambayo ipo hatua ya usafi baada ya kukamilika.
“Nimeridhishwa sana na ujenzi wa miradi hii na naahidi kuisimamia kwa karibu zaidi ili ifaidishe wananchi hasa wenye kipato cha chini” alisema Mkurugenzi Kihamia.
Aidha aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ni mafanikio ya utekelezaji wa ahadi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli pamoja na ilani ya CCM ya 2015 hadi 2020.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa