Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta akifanya mazungumzo na uongozi wa baraza la Wazee Wilaya ya Arusha tarehe 20/07/2020 katika ukumbi wa mikutano Shule ya msingi Arusha.
Mhe. Kimanta amesisitiza kuwa Wazee ni hazina na Taifa na nguzo muhimu katika ustawi wa Wilaya na Mkoa kiujumla hivyo ni muhimu kuzingatia sera za wazee zilizowekwa na Serikali yetu ili kuweza kuwatunza wazee.
Viongozi hao waliweza kuwasilisha maoni yao juu ya namna gani Serikali iweke uzito katika kulea kundi la wazee pamoja na namna bora ya Serikali kufikia mahitaji yao.
Katika kikao hiki Mhe. Kimanta aliongozana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Kheri Kagya
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa